Grade 4 Kiswahili Scheme of Work — Terms 1, 2 and 3, 2026
A CBE Kiswahili scheme of work for Grade 4 covering Terms 1, 2 and 3 2026: strands and sub-strands mapped week by week with specific learning outcomes, key inquiry questions, suggested learning experiences, resources and assessment methods.
- Level
- Grade 4
- Subject
- Kiswahili
- Terms
- Terms 1, 2 and 3
- Year
- 2026
- Weeks
- 39
Term 1 — Grade 4 Kiswahili scheme of work
13 weeks · first 5 freeStrands and sub-strands covered
| Wiki | Somo | Mada | Mada Ndogo | Matokeo Maalum Yanayotarajiwa | Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji | Swali Dadisi | Rasilimali za Ujifunzaji | Mbinu za Tathmini | Tafakari |
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | 1 | Kusikilizana Kuzungumza | Matamshi Bora | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua silabi zinazotokana na sauti p/b, t/d, k/g, ch/j katika maneno. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua silabi za sauti lengwa (p/b, t/d, k/g, ch/j) kutokana na maneno kwenye vitabu, ubaoni au kwa kutumia vifaa vya kidijitali; kusikiliza silabi za sauti lengwa zikitamkwa na mwalimu, mgeni mwalikwa au kutoka kwa vifaa vya kidijitali k.v. kinasasauti na rununu. | Matamshi bora yana umuhimu gani katika mawasiliano? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 2 | Kusikilizana Kuzungumza | Matamshi Bora | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutamka silabi zinazotokana na sauti zinazokaribiana kimatamshi. | Mwanafunzi aelekezwe: kutamka silabi za sauti lengwa na vitanzandimi akiwa na wenzake; kusikiliza vitanzandimi vilivyoundwa kutokana na maneno yenye sauti lengwa vikikaririwa na mwalimu, mgeni mwalikwa au katika vifaa vya kidijitali (k.m. baba alivua papa katika bahari pana, kila Chacha akila hali chakula kikichacha). | Matamshi bora yana umuhimu gani katika mawasiliano? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 3 | Kusikilizana Kuzungumza | Matamshi Bora | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutamka vitanzandimi vinavyoundwa kwa silabi za sauti zinazokaribiana kimatamshi; kuunda vitanzandimi kutokana na sauti zinazokaribiana kimatamshi. | Mwanafunzi aelekezwe: kuunda vitanzandimi vyepesi vinavyotokana na vitate husika akiwa na wenzake. | Matamshi bora yana umuhimu gani katika mawasiliano? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 4 | Kusikilizana Kuzungumza | Matamshi Bora | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia kukariri vitanzandimi vinavyoundwa kwa silabi za sauti zinazokaribiana kimatamshi katika kuboresha matamshi yake. | Mwanafunzi aelekezwe: kuunda vitanzandimi kwenye vifaa vya kidijitali na kushirikiana na wenzake mitamboni kuvirekebisha; kushiriki majadiliano kuhusu sababu za kukariri vitanzandimi maishani mwake. | Matamshi bora yana umuhimu gani katika mawasiliano? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 1 | Kusoma | Kusoma kwa Ufahamu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua msamiati wa mada lengwa uliotumika katika kifungu cha hadithi ili kuimarisha ufahamu; kutumia msamiati lengwa kwa usahihi katika sentensi. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua msamiati wa nyumbani (k.v. meza, sebule, balbu/globu, kizingiti, fremu, neti, tendegu, mtoto wa meza, mvungu, figa, kinu, tumbuu, kochi, kupiga deki) uliotumiwa katika kifungu cha hadithi; kushirikiana na wenzake kujadili maana na matumizi ya msamiati lengwa katika sentensi; kuimba nyimbo zinazolenga msamiati lengwa; kusoma kifungu kinachohusiana na suala lengwa kwenye kitabu au kwenye tarakilishi akiwa na wenzake. | Unazingatia nini ili kupata ujumbe katika kifungu cha hadithi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 2 | Kusoma | Kusoma kwa Ufahamu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutoa muhtasari wa ujumbe wa kifungu cha hadithi; kujenga mazoea ya usomaji bora katika maisha ya kila siku. | Mwanafunzi aelekezwe: kujibu maswali kutokana na kifungu alichosoma; kutoa muhtasari wa ujumbe wa kifungu alichokisoma; kumweleza mzazi au mlezi wake ujumbe wa kifungu alichokisoma. | Unazingatia nini ili kupata ujumbe katika kifungu cha hadithi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 3 | Kuandika | Kuandika Insha ya Wasifu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua insha ya wasifu kwa kuzingatia muundo; kuandika insha ya wasifu kwa kuzingatia ujumbe, mtindo na muundo ufaao. | Mwanafunzi aelekezwe: kujadili na wenzake maana ya insha ya wasifu; kutambua insha ya wasifu kwa kurejelea vielelezo vya insha vilivyoandikwa kwenye matini mbalimbali au tarakilishi; kujadili na wenzake mada ya insha na muundo wa insha ya wasifu akiwa. | Je, unazingatia mambo gani unapoandika insha nzuri ya wasifu? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 4 | Kuandika | Kuandika Insha ya Wasifu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia utunzi mzuri wa insha ya wasifu ili kujenga ubunifu wake. | Mwanafunzi aelekezwe: kuandaa vidokezo vitakavyomwongoza kuandika insha yake; kuandika insha inayoeleza sifa za mtu kama vile mzazi au mlezi, rafiki, mwalimu au kiongozi yeyote kwa kuzingatia anwani, mpangilio mzuri wa mawazo, hati nadhifu, tahajia, kanuni za kisarufi, uakifishaji mwafaka na kwa ubunifu; kuandika insha ya wasifu mtandaoni na kuisambaza kwa wenzake na mwalimu ili waisome na kuitathmini. | Je, unazingatia mambo gani unapoandika insha nzuri ya wasifu? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 1 | Sarufi | Nomino | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kueleza maana ya nomino ili kuitofautisha na aina nyingine za maneno; kutambua nomino katika kundi la maneno na sentensi. | Mwanafunzi aelekezwe: kushirikiana na wenzake kueleza maana ya nomino; kutambua nomino katika matini mbalimbali; kushirikiana na wenzake kutoa mifano ya nomino. | Je, ni vitu gani unavyoweza kupata katika mazingira yako? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 2 | Sarufi | Nomino | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia nomino kwa njia sahihi katika sentensi; kuonea fahari matumizi ya nomino katika mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kuchagua nomino kwenye tarakilishi, kuziburura na kuzitia kapuni akiwa na wenzake; kutumia nomino kujaza nafasi katika sentensi; kutumia nomino kutunga sentensi kwenye daftari na mtandaoni ili wenzake wazisome na kuzisahihisha. | Je, ni vitu gani unavyoweza kupata katika mazingira yako? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 3 | Sarufi | Vitenzi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kueleza maana ya vitenzi ili kuvitofautisha na aina nyingine za maneno; kutambua vitenzi katika kundi la maneno na sentensi. | Mwanafunzi aelekezwe: kushirikiana na wenzake kwa amani kueleza maana ya vitenzi; kushirikiana na wenzake kutoa mifano ya vitenzi (k.v. soma, andika, keti, simama, cheka) katika kadi za maneno, kapu maneno, ubao, vifaa vya kidijitali n.k; kutambua vitendo vinavyofanyika katika picha au michoro. | Ni shughuli gani unazofanya kila siku? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 4 | Sarufi | Vitenzi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia vitenzi ipasavyo katika mawasiliano; kuonea fahari. | Mwanafunzi aelekezwe: kuigiza vitenzi mbalimbali akishirikiana na wenzake; kutumia vitenzi kujaza nafasi kwenye sentensi na kifungu kifupi; kutumia vitenzi mbalimbali kutunga sentensi daftarini au mtandaoni kwa kuzingatia suala. | Ni shughuli gani unazofanya kila siku? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 1 | Sarufi | Vivumishi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kueleza maana ya kivumishi ili kukitofautisha na aina nyingine za maneno; kutambua vivumishi katika kundi la maneno na sentensi. | Mwanafunzi aelekezwe: kushirikiana na wenzake kueleza maana ya kivumishi; kutambua vivumishi katika kundi la maneno aliyopewa (k.m. -zuri, -baya, - refu, -fupi, -eusi, -eupe, n.k). | Ni sifa zipi unazoweza kutambua katika nomino mbalimbali? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 2 | Sarufi | Vivumishi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia vivumishi ipasavyo katika sentensi na kifungu; kuonea fahari matumizi ya. | Mwanafunzi aelekezwe: kuchagua vivumishi kwenye tarakilishi, kuviburura na kuvitia kapuni akiwa na wenzake; kutumia vivumishi kujaza nafasi katika sentensi; kutumia vivumishi kutunga sentensi daftarini na mtandaoni akizingatia. | Ni sifa zipi unazoweza kutambua katika nomino mbalimbali? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 3 | Kusikilizana Kuzungumza | Maamkuzi na Maagano | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua aina mbalimbali za maamkuzi na maagano katika mawasiliano; kueleza maamkuzi na maagano yanayotumika katika miktadha mbalimbali. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua maamkuzi (k.v. U mzima? U hali gani? Alamsiki, Lala unono, Siku njema) kutoka kwenye chati, ubao au vifaa vya kidijitali, michoro na picha; kushiriki mjadala na mwenzake kuhusu maamkuzi na maagano yanayolengwa na matumizi yake; kushirikiana na wenzake kuigiza maamkuzi na maagano lengwa. | Je, watu husalimiana na kuagana vipi katika jamii yako?; Kuamkua na kuaga watu kuna umuhimu gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 4 | Kusikilizana Kuzungumza | Maamkuzi na Maagano | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia aina mbalimbali za maamkuzi na maagano katika mawasiliano; kuchangamkia maamkuzi na maagano katika mahusiano. | Mwanafunzi aelekezwe: kutazama watu wakiamkuana na kuagana katika vifaa vya kidijitali; kuambatanisha maamkuzi na maagano na majibu sahihi daftarini au kwenye tarakilishi; kujadiliana na mzazi au mlezi wake kuhusu maamkuzi na maagano yanayotumiwa katika jamii yao. | Je, watu husalimiana na kuagana vipi katika jamii yako?; Kuamkua na kuaga watu kuna umuhimu gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 1 | Kusoma | Matumizi ya Kamusi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kueleza maana ya kamusi ili kuitofautisha na vitabu vingine; kutumia kamusi ipasavyo kutafuta maana za maneno asiyoyajua ili kukuza msamiati wake. | Mwanafunzi aelekezwe: kujadiliana na wenzake kuhusu maana na matumizi ya kamusi; kujadiliana na wenzake kuhusu mpangilio wa maneno katika kamusi. | Unazingatia nini unapotafuta maneno katika kamusi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 2 | Kusoma | Matumizi ya Kamusi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia umuhimu wa kamusi katika kukuza msamiati wake. | Mwanafunzi aelekezwe: kutumia kamusi kutafuta maana za maneno mbalimbali akiwa na wenzake; kutumia mtandao kusikiliza na kusoma maelezo kuhusu msamiati anaotafutia maana. | Unazingatia nini unapotafuta maneno katika kamusi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 3 | Kuandika | Insha ya Masimulizi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua insha ya masimulizi kwa kuzingatia muundo; kuandika insha ya masimulizi inayozingatia mada, ujumbe, mtindo na muundo ufaao. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua insha ya masimulizi kwa kurejelea vielelezo vya insha zilizoandikwa kwenye matini mbalimbali au tarakilishi; kushiriki na wenzake kujadili mada ya insha na muundo wa insha ya masimulizi. | Insha ya masimulizi inahusu nini?; Je, unazingatia nini unapoandika insha ya masimulizi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 4 | Kuandika | Insha ya Masimulizi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia utunzi mzuri wa insha ya masimulizi ili kukuza ubunifu wake. | Mwanafunzi aelekezwe: kuandaa vidokezo vitakavyomwongoza kuandika insha yake; kuandika insha inayosimulia kisa kinachohusu nidhamu mezani kwa kuzingatia anwani, mpangilio mzuri wa mawazo, hati safi, tahajia, kanuni za kisarufi, uakifishaji mwafaka na kwa lugha ya kiubunifu; kuwasomea wenzake insha aliyoandika ili waitathmini. | Insha ya masimulizi inahusu nini?; Je, unazingatia nini unapoandika insha ya masimulizi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review |
Weeks 6–13 are in the full Term 1 document — KES 30 by M-Pesa.
Term 2 — Grade 4 Kiswahili scheme of work
13 weeks · first 5 freeStrands and sub-strands covered
| Wiki | Somo | Mada | Mada Ndogo | Matokeo Maalum Yanayotarajiwa | Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji | Swali Dadisi | Rasilimali za Ujifunzaji | Mbinu za Tathmini | Tafakari |
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | 1 | Kuandika | Kuandika Barua ya Kirafiki | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua barua ya kirafiki kwa kuzingatia muundo wake; kujadili umuhimu wa barua ya kirafiki katika mawasiliano; kuandika barua ya kirafiki inayozingatia mada kwa kufuata kanuni zifaazo; kuchangamkia utunzi wa barua ya kirafiki katika mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua barua ya kirafiki kwa kurejelea vielelezo vya barua za kirafiki zilizoandikwa kwenye matini mbalimbali au tarakilishi; kujadiliana na wenzake kuhusu umuhimu wa barua za kirafiki katika mawasiliano; kujadili na wenzake mada ya barua ya kirafiki na vipengele vyake/ yale yanayofaa kujumuishwa; kuandaa vidokezo vitakavyomwongoza kuandika insha yake; kuandika barua ya kirafiki kwa rafiki, ndugu, mzazi, n.k kwa kuzingatia anwani, mpangilio mzuri wa mawazo, hati safi, tahajia, kanuni za kisarufi, uakifishaji mwafaka na kwa lugha ya kiubunifu; kuwasomea wenzake na mwalimu barua yake ili waitathmini. | Je, unazingatia nini ili kuandika barua nzuri ya kirafiki?; Barua za kirafiki inashughulikia masuala gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 2 | Sarufi | Ngeli ya A-WA | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi wa ngeli ya A-WA. | Mwanafunzi aelekezwe: kueleza maana ya ngeli za nomino akiwa na wenzake; kutaja mifano ya nomino akiwa na wenzake. | Ni nini kinakuwezesha kutambua nomino za ngeli ya A-WA? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 3 | Sarufi | Ngeli ya A-WA | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua nomino katika ngeli ya A-WA ili kuzitofautisha na nomino katika ngeli nyingine. | Mwanafunzi aelekezwe: kusoma sentensi zilizoundwa kutokana na nomino za ngeli ya A-WA katika umoja na wingi; kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi wa ngeli ya A-WA kwenye sentensi alizosoma. | Ni nini kinakuwezesha kutambua nomino za ngeli ya A-WA? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 4 | Sarufi | Ngeli ya A-WA | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuunda sentensi akitumia nomino za ngeli ya A-WA katika umoja na wingi akizingatia upatanisho wa kisarufi. | Mwanafunzi aelekezwe: kushiriki katika mchezo wa kuchopoa kadi za sentensi zenye nomino za ngeli ya A- WA kutoka kwenye kikapu au boksi na kisha kuzisoma; kutambua nomino za ngeli ya A-WA katika umoja na wingi katika matini; kujaza nafasi katika sentensi kwa kutumia viambishi vya umoja na wingi wa nomino katika ngeli ya A-WA. | Ni nini kinakuwezesha kutambua nomino za ngeli ya A-WA? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 1 | Sarufi | Ngeli ya A-WA | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia kutumia nomino za ngeli ya A-WA katika mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kuunda sentensi sahihi daftarini au kwenye kifaa cha kidijitali akitumia nomino za ngeli ya A- WA katika umoja na wingi akizingatia upatanisho wa kisarufi; kuwasomea au kuwazambazia wenzake na mwalimu sentensi alizozitunga ili kuzitathmini. | Ni nini kinakuwezesha kutambua nomino za ngeli ya A-WA? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 2 | Kusikiliza na Kuzungumza | Methali | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua methali zinazohusu malezi katika matini tofautitofauti; kueleza maana za methali kuhusu malezi. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua methali kuhusu malezi (k.v. mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, mtoto wa nyoka ni nyoka na mtoto hutazama kisogo cha nina) kutoka kwa orodha ya methali, chati au mtandaoni; kueleza maana za methali kuhusu malezi akiwa na wenzake. | Ni methali gani zinazohusu malezi?; Methali hutumiwa kufanya nini? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 3 | Kusikiliza na Kuzungumza | Methali | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia methali zinazohusu malezi katika mawasiliano; kuchangamkia matumizi ya methali katika miktadha mbalimbali. | Mwanafunzi aelekezwe: kukamilisha methali kuhusu malezi; kutumia methali kuhusu malezi katika kifungu kifupi na masimulizi akiwa na wenzake; kushirikiana na mzazi au mlezi wake kutambua methali kuhusu malezi katika jamii yao. | Ni methali gani zinazohusu malezi?; Methali hutumiwa kufanya nini? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 4 | Kusoma | Kusoma kwa Ufahamu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kueleza maana ya shairi, ubeti na mshororo ili kuvibainisha; kusoma shairi kwa ufasaha kwa kuzingatia ujumbe. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua shairi, beti na mishororo katika matini mbalimbali kama vile vitabu, chati na vilevile kwa kutumia tarakilishi; kushiriki katika majadiliano kuhusu maana za shairi, ubeti na mishororo; kusoma akizingatia msamiati wa mada lengwa; kusikiliza mashairi yanayokaririwa kwenye vifaa vya kidijitali. | Unaufahamu msamiati gani wa ushairi?; Mashairi yanaweza kuwasilisha ujumbe gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 1 | Kusoma | Kusoma kwa Ufahamu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua beti na mishororo katika shairi; kutambua shairi kutokana na umbo lake; kufurahia kutumia lugha ya ushairi anapozungumzia ushairi. | Mwanafunzi aelekezwe: kusoma au kukariri shairi kwa mahadhi mbalimbali akizingatia ujumbe; kushiriki mjadala kuhusu ujumbe unaojitokeza kwenye shairi; kusoma mashairi kwenye mitandao. | Unaufahamu msamiati gani wa ushairi?; Mashairi yanaweza kuwasilisha ujumbe gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 2 | Kuandika | Kuandika Insha ya Maelezo | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua vifungu vya maelezo katika matini; kuandika insha ya maelezo kwa kufuata kanuni zifaazo. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua vifungu vya maelezo vilivyoandikwa kwenye matini mbalimbali au tarakilishi; kuandaa vidokezo vitakavyomwongoza kuandika insha yake. | Insha ya maelezo inahusu nini?; Unazingatia nini unapoandika insha ya maelezo? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 3 | Kuandika | Kuandika Insha ya Maelezo | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia utunzi mzuri wa insha ya maelezo ili kujenga ubunifu wake. | Mwanafunzi aelekezwe: kuandika insha ya maelezo kuhusu mada lengwa (ushauri-nasaha) akitumia vivumishi na vielezi vifaavyo kutoa picha dhahiri kuhusu anachokielezea akizingatia anwani, mpangilio mzuri wa mawazo, hati safi, tahajia, kanuni za kisarufi, uakifishaji mwafaka na kwa lugha ya kiubunifu; kushiriki na wenzake kujadili mada ya insha na muundo wa insha ya maelezo; kuandika insha ya maelezo daftarini au kwenye kifaa cha kidijitali na kuwasomea au kuwasambazia wenzake na mwalimu ili kuitathmini. | Insha ya maelezo inahusu nini?; Unazingatia nini unapoandika insha ya maelezo? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 4 | Sarufi | Ngeli ya U-I | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi wa ngeli ya U-I. | Mwanafunzi aelekezwe: kusoma sentensi zilizoundwa kutokana na nomino za ngeli ya U-I katika umoja na wingi; kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi wa ngeli ya U-I kwenye sentensi alizosoma. | Nomino zinazorejelea mimea na vitu vya kimaumbile ni zipi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 1 | Sarufi | Ngeli ya U-I | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua nomino katika ngeli ya U-I ili kuzitofautisha na nomino katika ngeli nyingine. | Mwanafunzi aelekezwe: kushiriki katika mchezo wa kuchopoa kadi za sentensi zenye nomino za ngeli ya U-I kutoka kwenye kikapu au boksi na kisha kuzisoma; kutambua nomino katika ngeli ya U-I kwenye kadi, mti maneno, tarakilishi au kapu maneno. | Nomino zinazorejelea mimea na vitu vya kimaumbile ni zipi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 2 | Sarufi | Ngeli ya U-I | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuunda sentensi akitumia nomino za ngeli ya U-I, katika umoja na wingi akizingatia upatanisho wa kisarufi. | Mwanafunzi aelekezwe: kujaza nafasi katika sentensi kwa kutumia viambishi vya umoja na wingi wa nomino katika ngeli ya U-I. | Nomino zinazorejelea mimea na vitu vya kimaumbile ni zipi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 3 | Sarufi | Ngeli ya U-I | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia kutumia nomino za ngeli ya U-I katika mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kuunda sentensi sahihi daftarini au kwenye kifaa cha kidijitali akitumia nomino za ngeli ya U-I katika umoja na wingi akizingatia upatanisho wa kisarufi; kuwasomea au kuwazambazia wenzake na mwalimu sentensi alizozitunga ili kuzitathmini. | Nomino zinazorejelea mimea na vitu vya kimaumbile ni zipi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 4 | Kusikiliza na Kuzungumza | Kujieleza kwa Ufasaha | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kukariri au kuimba shairi kwa kuzingatia matamshi na mahadhi mbalimbali; kueleza maana ya msamiati uliotumiwa katika shairi. | Mwanafunzi aelekezwe: kukariri shairi kuhusu mada lengwa (bendera ya taifa) kwa kuzingatia matamshi na mahadhi mbalimbali; kusikilize shairi kuhusu suala lengwa likikaririwa au kuimbwa na mwalimu, mgeni mwalikwa (mghani) au kupitia vifaa vya kidijitali; kushirikiana na wenzake kukariri au kuimba shairi kwa mahadhi mbalimbali. | Ushairi unaweza kuboresha vipi mazungumzo yako? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 1 | Kusikiliza na Kuzungumza | Kujieleza kwa Ufasaha | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia msamiati uliotumiwa katika shairi ili kuboresha mawasiliano; kueleza ujumbe wa shairi ili kudhihirisha ufahamu wake; kuchangamkia ushairi kama njia ya kujieleza kwa ufasaha. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua msamiati uliotumika katika ushairi kuhusu maadili (k.v. uhuru, bendera, rangi za bendera, kupandisha na kushukisha bendera) na kuueleza akiwa peke yake au kwa kushirikiana na wenzake; kushirikiana na wenzake kujadili ujumbe katika shairi; kujibu maswali yanayotokana na shairi alilosikiliza, aliloimba au kukariri. | Ushairi unaweza kuboresha vipi mazungumzo yako? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 2 | Kusoma | Kusoma kwa Kina | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kusoma makala kwa kuzingatia vipengele mbalimbali vinavyoyajenga; kusoma na kutambua umuhimu wa ujumbe wa makala husika. | Mwanafunzi aelekezwe: kusoma makala ya aina mbalimbali (k.m. hadithi fupi, michezo mifupi, mashairi mafupi) akizingatia vipengele kama vile tahajia, sarufi, wahusika na ujumbe kutoka kwa kitabu, gazeti au blogi; kujadiliana na wenzake kuhusu makala aliyoyasoma na umuhimu wake. | Kusoma hadithi kuna umuhimu gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 3 | Kusoma | Kusoma kwa Kina | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kufurahia kusoma makala mbalimbali ili kukuza ufahamu. | Mwanafunzi aelekezwe: kutumia kamusi kupata maana za msamiati uliotumika katika makala. | Kusoma hadithi kuna umuhimu gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 4 | Kuandika | Kuandika Insha ya Wasifu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua insha ya wasifu kwa kuzingatia muundo; kuandika insha ya wasifu kwa kufuata kanuni zifaazo akizingatia vivumishi na vielezi kujenga picha dhahiri ya anachokielezea. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua insha ya wasifu kwa kurejelea vielelezo vya insha zilizoandikwa kwenye matini mbalimbali au tarakilishi; kuandaa vidokezo vitakavyomwongoza kuandika insha yake; kuandika insha inayoeleza sifa za mtu kama vile mzazi au mlezi, rafiki, mwalimu au kiongozi yeyote (kwa kutumia vivumishi na vielezi ili kujenga picha dhahiri ya anachokiandikia) daftarini kwa kuzingatia anwani, mpangilio mzuri wa mawazo, hati safi, tahajia, kanuni za kisarufi, uakifishaji mwafaka na kwa lugha ya kiubunifu. | Insha ya wasifu inahusu nini? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review |
Weeks 6–13 are in the full Term 2 document — KES 30 by M-Pesa.
Term 3 — Grade 4 Kiswahili scheme of work
13 weeks · first 5 freeStrands and sub-strands covered
| Wiki | Somo | Mada | Mada Ndogo | Matokeo Maalum Yanayotarajiwa | Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji | Swali Dadisi | Rasilimali za Ujifunzaji | Mbinu za Tathmini | Tafakari |
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | 1 | Kusikilizana Kuzungumza | Visawe | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kueleza maana ya kisawe ili kukibainisha; kutambua maneno mawili yenye maana sawa katika matini; kutumia visawe ifaavyo katika mawasiliano; kuthamini matumizi ya visawe katika mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kueleza maana ya neno kisawe akiwa na wenzake; kutambua maneno mawili ya kiwango chake yenye maana sawa (k.v. tembo, ndovu; kinyonga, lumbwi; adui, hasimu; siri, faragha; barua, waraka; ami-amu; televisheni, runinga) kwa kurejelea kapu maneno, kadi za maneno na mti maneno; kuambatanisha visawe kutoka kapu maneno, mti maneno, orodha ya maneno, chati, vyombo vya kidijitali au kadi za maneno; kutumia kisawe kimoja kuchukua nafasi ya kingine katika sentensi; kutumia kisawe kimoja kuchukua nafasi ya kingine katika kifungu kifupi. | Maneno yenye maana sawa yanasaidia vipi katika mawasiliano? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 2 | Kusoma | Kusoma kwa Ufahamu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kueleza maana ya mchezo wa kuigiza, mhusika na maelekezo; kutambua mchezo wa kuigiza katika matini. | Mwanafunzi aelekezwe: kushiriki katika majadiliano kuhusu maana za mchezo wa kuigiza, mhusika na maelekezo akiwa na wenzake; kutambua mchezo wa kuigiza, wahusika na maelekezo katika matini mbalimbali kama vile vitabu, chati na vilevile kwa kutumia tarakilishi. | Je, wahusika huchangia nini katika mchezo wa kuigiza? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 3 | Kusoma | Kusoma kwa Ufahamu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua wahusika na maelekezo katika mchezo mfupi wa kuigiza; kusoma mchezo mfupi wa kuigiza kwa ufasaha kwa kuzingatia ujumbe. | Mwanafunzi aelekezwe: atazame mchezo mfupi wa kuigiza ukiigizwa darasani au kwenye vifaa vya kidijitali; asome mchezo wa kuigiza akizingatia maelekezo na ujumbe; ashiriki mjadala kuhusu ujumbe unaojitokeza kwenye mchezo wa kuigiza. | Je, wahusika huchangia nini katika mchezo wa kuigiza? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 4 | Kusoma | Kusoma kwa Ufahamu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuigiza mchezo mfupi kwa kuzingatia maelekezo; kufurahia kusoma michezo na kuiigiza. | Mwanafunzi aelekezwe: asome mchezo wa kuigiza kwenye mtandao; ajibu maswali yanayotokana na mchezo wa kuigiza aliosoma. | Je, wahusika huchangia nini katika mchezo wa kuigiza? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 1 | Kuandika | Kuandika Insha ya Masimulizi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua insha ya masimulizi kwa kuzingatia muundo; kuandika insha ya masimulizi kwa kufuata kanuni zifaazo. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua insha ya masimulizi kwa kurejelea vielelezo vya insha zilizoandikwa kwenye matini mbalimbali au tarakilishi; kuandaa vidokezo vitakavyomwongoza kuandika insha yake; aandike insha inayosimulia kisa cha tukio linalohusiana na wanyama wa porini kwa kuzingatia anwani, mpangilio mzuri wa mawazo, hati safi, tahajia, kanuni za kisarufi, uakifishaji mwafaka na kwa lugha ya kiubunifu. | Insha ya masimulizi inahusu nini?; Je, unazingatia nini ili kuandika insha nzuri ya masimulizi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 2 | Kuandika | Kuandika Insha ya Masimulizi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia utunzi mzuri wa insha ya masimulizi ili kujenga ubunifu wake. | Mwanafunzi aelekezwe: ashiriki na wenzake kujadili mada ya insha na muundo wa insha ya masimulizi; aandike insha ya masimulizi mtandaoni na kuisambaza kwa wenzake na mwalimu ili waisome na kuitathmini; awasomee wenzake insha aliyoandika ili waisikilize na kuitathmini. | Insha ya masimulizi inahusu nini?; Je, unazingatia nini ili kuandika insha nzuri ya masimulizi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 3 | Sarufi | Mnyambuliko wa Vitenzi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kueleza maana ya mnyambuliko wa vitenzi ili kuubainisha; kueleza maana ya kauli za kutenda, kutendea na kutendwa ili kuzitofautisha. | Mwanafunzi aelekezwe: kushirikiana na wenzake kueleza maana za mnyambuliko wa vitenzi, kauli ya kutenda, kauli ya kutendea na kauli ya kutendwa; kutambua vitenzi katika kauli za kutenda, kutendea na kutendwa katika chati, jedwali, kapu maneno, mti maneno, ubao na vyombo vya kidijitali. | Je, vitenzi vinaweza kubadilika vipi mwishoni ili kuleta maana mbalimbali? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 4 | Sarufi | Mnyambuliko wa Vitenzi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua vitenzi katika kauli za kutenda, kutendea na kutendwa katika matini. | Mwanafunzi aelekezwe: anyambue vitenzi katika kauli lengwa akiwa peke yake, wakiwa wawili wawili au katika vikundi; atumie vitenzi katika kauli lengwa kwenye sentensi. | Je, vitenzi vinaweza kubadilika vipi mwishoni ili kuleta maana mbalimbali? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 1 | Sarufi | Mnyambuliko wa Vitenzi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia vitenzi katika kauli za kutenda, kutendea na kutendwa ipasavyo anapowasiliana; kuchangamkia matumizi ya vitenzi katika kauli za kutenda, kutendea na kutendwa kwenye mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kushirikiana na wenzake kujaza nafasi katika jedwali la mnyambuliko wa vitenzi kwenye daftari au kwa kutumia tarakilishi; kuandika sentensi upya kwa kutumia vitenzi katika kauli mbalimbali. | Je, vitenzi vinaweza kubadilika vipi mwishoni ili kuleta maana mbalimbali? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 2 | Kusikilizana Kuzungumza | Mazungumzo | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua miktadha ya mawasiliano isiyo rasmi; kutumia lugha ipasavyo katika miktadha isiyo rasmi. | Mwanafunzi aelekezwe: kushirikiana na wenzake kutaja miktadha ya mazungumzo yasiyo rasmi (k.v. wanapocheza, wanapozungumza na marafiki, wakiwa nyumbani, n.k); kutambua mazungumzo yasiyo rasmi kwa kutazama maigizo ya mazungumzo lengwa kwenye video na tarakilishi. | Ni lini tunatumia lugha isiyo rasmi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 3 | Kusikilizana Kuzungumza | Mazungumzo | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia matumizi ya lugha katika miktadha isiyo rasmi. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua umuhimu wa nidhamu ya lugha katika mazingira yasiyo rasmi (k.m. kutumia lugha ya upole, heshima na kumpa mwenzake nafasi ya kuzungumza na kusikiliza kwa makini anaposhiriki katika mazungumzo); kuigiza mazungumzo katika miktadha isiyo rasmi (k.m. akicheza na wenzake, akizungumza na wazazi, ndugu, nyanya au babu nyumbani) akiwa na wenzake. | Ni lini tunatumia lugha isiyo rasmi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 4 | Kusoma | Kusoma kwa Mapana | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua matini ya kusoma ya aina mbalimbali na kuchagua zinazomvutia. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua matini (k.v. vitabu, majarida, magazeti) yanayovutia maktabani na mtandaoni. | Kusoma matini mbalimbali kuna umuhimu gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 1 | Kusoma | Kusoma kwa Mapana | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kusoma matini aliyochagua ili kufaidi ujumbe na lugha iliyotumiwa. | Mwanafunzi aelekezwe: asome matini aliyochagua (yakijumuisha yale yenye mada ya afya bora) ili kufaidi ujumbe na lugha iliyotumiwa; awasimulie wenzake kuhusu matini aliyosoma ili kupashana ujumbe na kuchocheana kusoma zaidi kwa ajili ya kujifurahisha. | Kusoma matini mbalimbali kuna umuhimu gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 2 | Kusoma | Kusoma kwa Mapana | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kufurahia usomaji wa aina mbalimbali za matini ili kupanua mawazo yake. | Mwanafunzi aelekezwe: ajadiliane na wenzake matini ambayo wamesoma. | Kusoma matini mbalimbali kuna umuhimu gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 3 | Kuandika | Insha ya Maelezo | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua insha ya maelezo katika matini; kuandika insha ya maelezo kwa kufuata kanuni zifaazo. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua vifungu vya maelezo vilivyoandikwa kwenye matini mbalimbali au tarakilishi; kuandaa vidokezo vitakavyomwongoza kuandika insha yake; kuandika insha ya maelezo akitumia lugha ifaayo kutoa picha dhahiri kuhusu anachokieleza; kuandika insha ya maelezo akizingatia anwani, mpangilio mzuri wa mawazo, hati safi, tahajia, kanuni za kisarufi, uakifishaji mwafaka na lugha ya kiubunifu inayojumuisha methali na nahau alizojifunza awali. | 1) Je, ni vitu gani vinavyoweza kutungiwa insha ya maelezo? 2) Ni mambo gani unayostahili kuzingatia unapoandika insha ya maelezo? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 4 | Kuandika | Insha ya Maelezo | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia utunzi wa insha ya maelezo ili kujenga ubunifu wake. | Mwanafunzi aelekezwe: kushiriki na wenzake kujadili mada ya insha (ihusiane na mada ya afya bora) na muundo wa insha ya maelezo; kuandika insha ya maelezo mtandaoni na kuisambaza kwa wenzake na mwalimu ili waisome na kuitathmini; kuwasomea wenzake insha aliyoandika ili waisikilize na kuitathmini. | 1) Je, ni vitu gani vinavyoweza kutungiwa insha ya maelezo? 2) Ni mambo gani unayostahili kuzingatia unapoandika insha ya maelezo? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 1 | Sarufi | Vinyume vya Nomino | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kueleza maana ya kinyume cha nomino ili kukibainisha; kutambua vinyume vya nomino katika matini. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua vinyume vya nomino (k.v. rafiki – adui, mgeni – mwenyeji, furaha – huzuni, uhuru-utumwa, mfalme-malkia, usiku – mchana, tajiri – maskini, n.k) katika chati, kadi za maneno, kapu maneno, mti maneno au vifaa vya kidijitali; kushirikiana na wenzake kutafuta vinyume vya nomino kwa kurejelea orodha ya nomino alizopewa. | Matumizi ya vinyume vya nomino huchangia vipi katika ukuzaji wa lugha? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 2 | Sarufi | Vinyume vya Nomino | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuunda sentensi kwa kutumia vinyume vya nomino ipasavyo; kuchangamkia matumizi ya vinyume vya nomino katika mawasiliano ya kila siku. | Mwanafunzi aelekezwe: kutalii mazingira yake na kuunda orodha ya vinyume vya nomino za vitu halisi anavyoweza kutambua; kutunga sentensi kwa kutumia vinyume vya nomino kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi. | Matumizi ya vinyume vya nomino huchangia vipi katika ukuzaji wa lugha? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 3 | Kusikilizana kuzungumza | Tashbihi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kueleza maana ya tashbihi ili kuibainisha; kutambua tashbihi za kimo na umbo katika matini. | Mwanafunzi aelekezwe: kushirikiana na wenzake kuelezea maana ya tashbihi; kutambua tashbihi za kimo na umbo (k.v. mrefu kama twiga, mfupi kama nyundo, mwembamba kama sindano, konda kama ng’onda) katika vitabu, chati na vyombo vya kidijitali. | Matumizi ya tashbihi yana umuhimu gani katika mawasiliano? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 4 | Kusikilizana kuzungumza | Tashbihi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia tashbihi za kimo na umbo kwa usahihi katika sentensi; kufurahia matumizi ya tashbihi za kimo na umbo katika mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kurejelea picha au michoro kwenye chati au tarakilishi ili kutumia tashbihi zifaazo kutolea maelezo; kutunga sentensi akitumia tashbihi za kimo na umbo akiwa peke yake au katika vikundi; kukamilisha sentensi zinazolinganisha vitu viwili kwa kutumia tashbihi za kimo na umbo. | Matumizi ya tashbihi yana umuhimu gani katika mawasiliano? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review |
Weeks 6–13 are in the full Term 3 document — KES 30 by M-Pesa.
More Grade 4 schemes of work
Questions about this scheme of work
Does this page cover all the terms?
It carries Terms 1, 2 and 3 of 2026 — every term published for Grade 4 Kiswahili so far. Each term has its own week-by-week table and free preview, and a new term joins this same page when it goes live.
How do I download a whole term as a PDF?
The first 5 weeks of each term are free to read on this page. Open the term you need, pay KES 30 by M-Pesa, then use Print / Save PDF — the sheet is laid out for A4 landscape.
Can I adapt it for my own school calendar?
Every scheme is generated from the curriculum taxonomy, so you can rebuild it with your own week count, strands and pacing on the Generate screen and keep the result as your own document.