Grade 6 Kiswahili Scheme of Work — Terms 1, 2 and 3, 2026
A CBE Kiswahili scheme of work for Grade 6 covering Terms 1, 2 and 3 2026: strands and sub-strands mapped week by week with specific learning outcomes, key inquiry questions, suggested learning experiences, resources and assessment methods.
- Level
- Grade 6
- Subject
- Kiswahili
- Terms
- Terms 1, 2 and 3
- Year
- 2026
- Weeks
- 39
Term 1 — Grade 6 Kiswahili scheme of work
13 weeks · first 5 freeStrands and sub-strands covered
| Wiki | Somo | Mada | Mada Ndogo | Matokeo Maalum Yanayotarajiwa | Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji | Swali Dadisi | Rasilimali za Ujifunzaji | Mbinu za Tathmini | Tafakari |
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | 1 | Kusikiliza na Kuzungumza | Matamshi Bora | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua silabi zinazotokana na sauti d/nd, ch/sh, j/nj na g/ng katika maneno. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua silabi za sauti, d/nd, ch/sh, j/nj na g/ng (k.v. doa/ndoa, choka/shoka, jaa/njaa, goma/ngoma) kutokana na maneno kwenye vitabu, ubaoni au kwa kutumia vifaa vya kidigitali; kusikiliza silabi za sauti lengwa zikitamkwa na mwalimu, mgeni mwalikwa au kutoka kwa vifaa vya kidigitali (k.v. kinasasauti). | Je, unajua maneno gani yenye silabi za sauti d/nd, ch/sh, j/nj na g/ng?; Je, Unajua vitanzandimi gani vyenye silabi za sauti d/nd, ch/sh, j/nj na g/ng? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 2 | Kusikiliza na Kuzungumza | Matamshi Bora | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutamka silabi zinazotokana na sauti zinazokaribiana kimatamshi ili kuimarisha matamshi. | Mwanafunzi aelekezwe: kutamka silabi za sauti lengwa akishirikiana na wenzake; kusikiliza vitanzandimi vinavyoundwa kutokana na maneno yenye sauti lengwa vikikaririwa (k.v. Mkunjo ulikunjwa na waja wenye njaa kukicha). | Je, unajua maneno gani yenye silabi za sauti d/nd, ch/sh, j/nj na g/ng?; Je, Unajua vitanzandimi gani vyenye silabi za sauti d/nd, ch/sh, j/nj na g/ng? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 3 | Kusikiliza na Kuzungumza | Matamshi Bora | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutamka vitanzandimi vinavyoundwa kwa silabi za sauti zinazokaribiana kimatamshi ili kuimarisha matamshi bora. | Mwanafunzi aelekezwe: kuunda vitanzandimi vinavyotokana na vitate husika akishirikiana na wenzake; kuwasilisha vitanzandimi alivyounda darasani ili wenzake wamtolee maoni. | Je, unajua maneno gani yenye silabi za sauti d/nd, ch/sh, j/nj na g/ng?; Je, Unajua vitanzandimi gani vyenye silabi za sauti d/nd, ch/sh, j/nj na g/ng? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 4 | Kusikiliza na Kuzungumza | Matamshi Bora | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia kukariri vitanzandimi vinavyoundwa kwa silabi za sauti zinazokaribiana kimatamshi ili kuimarisha matamshi. | Mwanafunzi aelekezwe: kutoa maoni kuhusu vitanzandimi vya wenzake kwa upendo na heshima; kuunda vitanzandimi kwenye vifaa vya kidijitali kwa kushirikiana na wenzake mitamboni na kuvirekebisha. | Je, unajua maneno gani yenye silabi za sauti d/nd, ch/sh, j/nj na g/ng?; Je, Unajua vitanzandimi gani vyenye silabi za sauti d/nd, ch/sh, j/nj na g/ng? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 1 | Kusoma | Kusoma kwa Ufahamu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua msamiati wa suala lengwa uliotumika katika kifungu ili kuimarisha ufahamu; kueleza maana ya msamiati lengwa ili kuubainisha. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua viungo vya mwili vya ndani (k.v. moyo, mapafu, ini, kibofu, wengu, figo, ubongo, mifupa na mishipa) kutokana na picha, chati au kwenye tarakilishi; kueleza maana za msamiati alioutambua; kusoma kifungu kuhusu suala lengwa kwenye kitabu au kwenye tarakilishi akishirikiana na wenzake; kujibu maswali kutokana na kifungu husika. | Unazingatia nini unaposoma kifungu cha hadithi?; Kusoma kuhusu viungo vya mwili vya ndani kuna umuhimu gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 2 | Kusoma | Kusoma kwa Ufahamu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuonyesha ufahamu wa kifungu kwa kujibu maswali na kutoa muhtasari; kuchangamkia usomaji ili kuimarisha ufahamu. | Mwanafunzi aelekezwe: kutoa muhtasari wa kifungu alichosoma; kutunga sentensi akitumia msamiati wa suala lengwa uliotumiwa katika kifungu, akishirikiana na wenzake; kusoma vifungu mtandaoni kuhusu suala lengwa akisaidiwa na mzazi au mlezi wake, kuwasilisha kwa wenzake ujumbe alioupata katika vifungu alivyovisoma. | Unazingatia nini unaposoma kifungu cha hadithi?; Kusoma kuhusu viungo vya mwili vya ndani kuna umuhimu gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 3 | Kuandika | Insha ya Wasifu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kujadili maudhui ya insha ya wasifu kwa kuzingatia mada ili kukuza ubunifu; kuandika insha ya wasifu kwa ubunifu ili kujenga maelezo yenye kutoa picha dhahiri. | Mwanafunzi aelekezwe: kusoma vielelezo vya insha ya wasifu vilivyoandikwa katika matini mbalimbali au tarakilishi huku akitambua maudhui; kujadili mada na muundo wa insha ya wasifu; kubainisha na kujadili vidokezo vifaavyo vya mada lengwa; kujadili maudhui ya insha ya wasifu kwa kurejelea mada. | Je, wasifu hueleza kuhusu nini? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 4 | Kuandika | Insha ya Wasifu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia utunzi wa insha ya wasifu ili kujenga ubunifu. | Mwanafunzi aelekezwe: kuandika insha ya wasifu isiyopungua maneno 200 inayohusu mada lengwa (k.m: Daktari nimpendaye) kwa kuzingatia, anwani, mpangilio mzuri wa mawazo, hati safi, kanuni za kisarufi (k.v. uakifishaji mwafaka na tahajia) na kwa lugha ya kiubunifu inayojumuisha methali, tashbihi na nahau alizojifunza awali; kukuza umilisi wa ujuzi wa kidijitali kwa kuandika insha ya wasifu mtandaoni na kuisambaza kwa wenzake na mwalimu ili kuisoma na kuitathmini; kuwawasilishia wenzake insha aliyoandika ili wampe maoni yao. | Je, wasifu hueleza kuhusu nini? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 1 | Sarufi | Vivumishi vya Sifa | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kueleza maana ya vivumishi vya sifa ili kuvitofautisha na aina zingine za maneno; kutambua vivumishi vya sifa katika matini mbalimbali ili kuvibainisha. | Mwanafunzi aelekezwe: kueleza maana ya vivumishi lengwa kwa kurejelea vitu au watu katika mazingira yake (k.m.: Mwalimu mzuri, njia ndefu, kijiko kichafu); kutambua vivumishi vya sifa (k.v. – zuri, -baya, -refu, -fupi, - ekundu, hodari) katika tarakilishi, kapu la maneno au mti wa maneno akishirikiana na wenzake; kutambua vivumishi vya sifa katika sentensi. | Ni maneno gani unayotumia kuelezea sifa za watu au kitu? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 2 | Sarufi | Vivumishi vya Sifa | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia vivumishi vya sifa kutunga sentensi au vifungu vya maneno kwa usahihi; kufurahia kutumia vivumishi vya sifa katika sentensi au vifungu vya maneno. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua vivumishi vya sifa katika kifungu; kuandika sentensi kwa usahihi akitumia vivumishi lengwa akishirikiana na wenzake; kujaza nafasi kwenye sentensi au vifungu vya maneno kwa kutumia vivumishi lengwa kwenye daftari au kwenye tarakilishi. | Ni maneno gani unayotumia kuelezea sifa za watu au kitu? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 3 | Sarufi | Vivumishi Viashiria | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kueleza maana ya vivumishi viashiria ipasavyo ili kuvibainisha; kutambua vivumishi viashiria katika matini mbalimbali. | Mwanafunzi aelekezwe: kueleza maana ya vivumishi lengwa kwa kurejelea vitu vilivyo karibu naye, mbali naye na mbali kabisa (k.m: Kitabu hiki/hicho/kile); kutambua vivumishi viashiria (k.v. huyu, huyo, yule, hivi, hivyo, vile) katika tarakilishi, kapu la maneno au mti wa maneno ili kukuza hamu ya ujifunzaji; kutambua vivumishi viashiria katika sentensi; kutambua vivumishi katika kifungu. | Ni maneno gani unayoweza kutumia kuonyesha umbali wa mtu au kitu? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 4 | Sarufi | Vivumishi Viashiria | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia vivumishi viashiria katika sentensi au vifungu vya maneno kwa usahihi; kufurahia kutumia vivumishi viashiria katika sentensi au vifungu vya maneno. | Mwanafunzi aelekezwe: kuandika sentensi akitumia vivumishi lengwa kwa usahihi akishirikiana na wenzake; kujaza mapengo kwenye sentensi au vifungu vya maneno kwa kutumia vivumishi lengwa; kutunga sentensi sahihi au vifungu vya maneno katika kifaa cha kidijitali akitumia vivumishi lengwa. | Ni maneno gani unayoweza kutumia kuonyesha umbali wa mtu au kitu? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 1 | Sarufi | Vivumishi Vimilikishi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuelezea maana ya vivumishi vimilikishi ili kuvitofautisha na aina zingine za vivumishi; kutambua vivumishi vimilikishi katika matini mbalimbali. | Mwanafunzi aelekezwe: kueleze maana ya vivumishi vimilikishi ili kuibainisha; kutambua vivumishi vimilikishi (k.v –angu, - ako, -ake, -etu, -ao n.k.) katika tarakilishi, kapu la maneno au mti wa maneno; kutambua vivumishi vimilikishi katika sentensi; kutambua vivumishi vimilikishi katika kifungu; kujadili maana vivumishi vimilikishi huko akitoa mifano. | Je, unajua maneno yapi yanayotumika Kuonyesha kitu ni cha nani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 2 | Sarufi | Vivumishi Vimilikishi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia vivumishi vimilikishi katika sentensi; kuonea fahari matumizi ya vivumishi vimilikishi katika mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kutumia vivumishi vimilikishi katika sentensi kwa kuigiza umiliki wa vitu mbalimbali; kutunga sentensi akitumia vivumishi vimilikishi; kukuza ujuzi wa kidijitali kwa kutumia vifaa vya kidijitali kutunga sentensi akitumia vivumishi vimilikishi na na kuzituma mtandaoni ili wenzake wazisome na kuzisahihisha; kujaza mapengo kwa kutumia vivumishi vimilikishi ili kukamilisha sentensi kwenye; daftari au katika tarakilishi kwa kuburura viwakilishi vimilikishi mwafaka. | Je, unajua maneno yapi yanayotumika Kuonyesha kitu ni cha nani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 3 | Kusikilizana Kuzungumza | Maamkuzi na Maagano | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kujadili umuhimu maamkuzi na maagano katika mawasiliano; kujadili maamkuzi na maagano yanayotumika katika miktadha mbalimbali. | Mwanafunzi aelekezwe: kujadili na wenzake umuhimu wa maamkuzi na maagano; kutambua maamkuzi mbalimbali (k.v. Waambaje? Salam Aleikum? Unaendeleaje?) na maagano mbalimbali (k.v. mchana mwema, buriani, baki salama) kutoka kwenye chati, ubao, michoro, picha au vifaa vya kidijitali. | Kwa nini watu huamkuana?; Kuagana kuna umuhimu gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 4 | Kusikilizana Kuzungumza | Maamkuzi na Maagano | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia aina mbalimbali za maamkuzi na maagano katika mawasiliano; kuchangamkia maamkuzi na maagano katika mahusiano. | Mwanafunzi aelekezwe: kujadili maamkuzi na maagano yanayolengwa na matumizi yake; kutazama watu wakiamkuana na kuagana katika vifaa vya kidijitali; kuigiza maamkuzi na maagano lengwa na kuheshimu nafasi ya kila mmoja katika maigizo haya. | Kwa nini watu huamkuana?; Kuagana kuna umuhimu gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 1 | Kusoma | Kusoma kwa Kina | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua maana, tahajia, ngeli na aina za maneno kwa kutumia kamusi; kutumia kamusi ipasavyo kutafuta maana za maneno mageni yaliyo katika matini aliyosoma ili kukuza msamiati wake. | Mwanafunzi aelekezwe: kushiriki katika mjadala na wenzake kuhusu jinsi ya kutumia kamusi kutambua maana, tahajia, ngeli, aina za maneno na maana za maneno hayo; kusikiliza msamiati wa suala lengwa (k.v. kambumbu, gori, hoki, Jugwe) ukisomwa na mwalimu, mgeni mwalikwa au katika kifaa cha kidijitali na kutambua tahajia yake kwa kutumia kamusi akishirikiana na wenzake; kuchagua maneno kutoka kapu maneno, mti maneno, kadi maneno au kifaa cha kidijitali na kutambua ngeli, aina na maana za maneno hayo kwa kurejelea kamusi akishirikiana na wenzake. | Unatafutaje maana ya maneno kwenye kamusi?; Kwa nini tunatumia kamusi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 2 | Kusoma | Kusoma kwa Kina | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia umuhimu wa kamusi katika kukuza msamiati na sarufi ya Kiswahili. | Mwanafunzi aelekezwe: kutumia kamusi kutafuta maana za maneno mbalimbali akishirikiana na wenzake; kutumia mtandao kutafuta maana za maneno; kutumia mtandao kusikiliza na kusoma maelezo kuhusu msamiati anaotafutia maana. | Unatafutaje maana ya maneno kwenye kamusi?; Kwa nini tunatumia kamusi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 3 | Kuandika | Insha za Masimulizi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kubainisha vidokezo vya kutumia katika kuandika insha ya masimulizi. | Mwanafunzi aelekezwe: kubainisha na kujadili vidokezo vifaavyo vya mada lengwa; kujadili mada na muundo wa insha ya masimulizi na kukuza umilisi wa mawasiliano na ushirikiano. | Je, unazingatia nini ili kuandika insha nzuri ya masimulizi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 4 | Kuandika | Insha za Masimulizi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuandika insha ya masimulizi kwa kuzingatia mtindo na muundo wake, kuchangamkia utunzi wa insha ya masimulizi ili kujenga ubunifu. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua insha ya masimulizi kwa kurejelea vielelezo vya insha zilizoandikwa kwenye matini mbalimbali au tarakilishi; kuandika insha isiyopungua maneno 200 inayosimulia kisa cha tukio linalohusiana na michezo kwa kuzingatia anwani, mpangilio mzuri wa mawazo, hati safi, tahajia, kanuni za kisarufi, uakifishaji mwafaka na kwa lugha ya kiubunifu. Katika kufanya hivi, atakuza ubunifu, kukuza ujuzi wa kidijitali kwa kuandika insha ya masimulizi mtandaoni na kuisambaza kwa wenzake na mwalimu ili kuisoma na kuitathmini, kuwawasilishia wenzake insha aliyoandika ili waitathmini. | Je, unazingatia nini ili kuandika insha nzuri ya masimulizi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review |
Weeks 6–13 are in the full Term 1 document — KES 30 by M-Pesa.
Term 2 — Grade 6 Kiswahili scheme of work
13 weeks · first 5 freeStrands and sub-strands covered
| Wiki | Somo | Mada | Mada Ndogo | Matokeo Maalum Yanayotarajiwa | Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji | Swali Dadisi | Rasilimali za Ujifunzaji | Mbinu za Tathmini | Tafakari |
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | 1 | Kusikiliza na Kuzungumza | Heshima, Adabu na Vyeo | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua maneno ya heshima yanayotumiwa katika mawasiliano; kuonyesha uelewa wa maneno ya heshima kwa kuyatumia kwa usahihi katika mawasiliano; kuthamini kutumia maneno ya heshima katika mawasiliano ya kila siku. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua maneno ya heshima (k.v. shehe, kasisi, padre, mwadhini, mheshimiwa, rais, mtawa) kwenye ubao, mti maneno, tarakilishi au kapu maneno; kueleza maana ya maneno lengwa kama yanavyotumiwa katika mahusiano ya kila siku kati ya watu; kutunga sentensi kwa kutumia maneno lengwa kwa usahihi; kutazama maigizo ya watu wakitumia maneno ya heshima kwenye tarakilishi na video; kuigiza mazungumzo mafupi akiwa na wenzake huku akitumia msamiati wa heshima. | Ni maneno yapi ya heshima unayoyajua na unayoweza kutumia kurejelea watu tofauti?; Kutumia maneno ya heshima kuna umuhimu gani katika jamii? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 2 | Kusoma | Kusoma kwa Mapana | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua hatua za kiusalama katika matumizi ya vifaa vya kidijitali anaposoma; kusakura matini kwenye tovuti salama ili kupata vifungu vya kusoma vyenye mada lengwa. | Mwanafunzi aelekezwe: kujadili na wenzake kuhusu hatua za kiusalama na maadili anayofaa kuzingatia anapotafuta na kusoma matini ya kidijitali; kujadili na wenzake kuhusu utunzaji wa vifaa vya kidijitali anavyotumia katika usomaji; kuzingatia hatua za kiusalama katika kutumia vifaa vya kidijitali (k.v. kufungua mitandao ifaayo); kutambua jina la faili lengwa kwenye tarakilishi na kufanya mazoezi ya kufungua na kufunga faili; kutambua mitandao salama yenye matini inayoafiki kiwango na mahitaji yake. | Kusoma matini ya kidijitali kuna manufaa gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 3 | Kusoma | Kusoma kwa Mapana | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia vifaa ya kidijitali kwa urahisi ili kupata matini yanayolengwa; kuchangamkia matumizi ya vifaa vya kidijitali katika kutafuta na kusoma ujumbe ili kuimarisha maarifa yake. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua umuhimu wa kutoa habari kwa mwalimu, mzazi au mlezi wake endapo atapata ujumbe kutoka kwa watu asiowajua mtandaoni na kutowasiliana nao; kusoma matini yanayojumuisha msamiati wa misimu kwa kutumia vifaa vya kidijitali; kutafuta maana za maneno mapya kwenye kamusi mtandaoni; kusikiliza matamshi na maelezo kuhusu anachokisoma mtandaoni panapowezekana; kutoa habari kwa muhtasari kuhusu matini aliyosoma na kujibu maswali katika maandishi au mazungumzo na wenzake. | Kusoma matini ya kidijitali kuna manufaa gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 4 | Kuandika | Barua Rasmi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua barua rasmi kwa kuzingatia muundo wake. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua barua rasmi kwenye kielelezo cha barua rasmi iliyochapishwa au kwenye tarakilishi. | Barua rasmi ni barua ya aina gani; Unazingatia nini unapoandika barua rasmi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 1 | Kuandika | Barua Rasmi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua vipengele vya barua rasmi ili kuvizingatia katika uandishi. | Mwanafunzi aelekezwe: kujadili vipengele vya barua rasmi (k.v. anwani ya mwandishi [jina, sanduku la posta, tarehe], anwani ya mpokeaji [cheo, sanduku la posta], mtajo, mada ya barua, mwili, hitimisho, sahihi na jina la mwandishi). | Barua rasmi ni barua ya aina gani; Unazingatia nini unapoandika barua rasmi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 2 | Kuandika | Barua Rasmi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuandika barua rasmi kwa kufuata kanuni zifaazo. | Mwanafunzi aelekezwe: kuandika barua rasmi kwa mwalimu akiomba kujiunga na klabu shuleni (k.v. vile skauti, mazingira,kilimo na muziki), akishirikiana na wenzake darasani, kwa hati za mkono au kwa kutumia kifaa cha kidijitali akizingatia muundo wa uandishi wa barua rasmi; kuandika barua rasmi katika daftari akiwa peke yake. | Barua rasmi ni barua ya aina gani; Unazingatia nini unapoandika barua rasmi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 3 | Kuandika | Barua Rasmi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia umuhimu wa barua rasmi katika mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kujadiliana na wenzake kuhusu umuhimu wa barua rasmi katika mawasiliano. | Barua rasmi ni barua ya aina gani; Unazingatia nini unapoandika barua rasmi? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 4 | Sarufi | Ngeli ya YA-YA | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya YA – YA katika sentensi. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua viambishi vya ngeli ya YA- YA katika sentensi kwa kuvipigia mstari au kuvikoleza rangi katika tarakilishi. | Je, unajua majina gani ya vitu visivyohesabika? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 1 | Sarufi | Ngeli ya YA-YA | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua nomino katika ngeli ya YA-YA kutokana na upatanisho wa kisarufi. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua nomino katika ngeli ya YA-YA kutokana naupatanisho wa kisarufi kwenye sentensi (k.m. maji, maziwa, mate, marashi na maskani). | Je, unajua majina gani ya vitu visivyohesabika? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 2 | Sarufi | Ngeli ya YA-YA | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia nomino za ngeli ya YA –YA katika umoja na wingi akizingatia upatanisho wa kisarufi. | Mwanafunzi aelekezwe: kuandika nomino katika ngeli ya YA-YA katika umoja na wingi akishirikiana na wenzake. | Je, unajua majina gani ya vitu visivyohesabika? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 3 | Sarufi | Ngeli ya YA-YA | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia kutumia nomino za ngeli ya YA- YA katika mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kutunga sentensi sahihi kwa kutumia nomino za ngeli ya YA-YA kwa kushirikiana na wenzake. | Je, unajua majina gani ya vitu visivyohesabika? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 4 | Kusikiliza Na Kuzungumza | Methali | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua methali zinazohusu umoja na ushirikiano katika matini; kueleza maana na matumizi ya methali mbalimbali zinazohusu umoja na ushirikiano katika jamii. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua methali zinazohusu umoja na ushirikiano (kama vile; umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, jifya moja haliinjiki chungu, kidole kimoja hakivunji chawa, kinga na kinga ndio moto huwaka n.k.) katika chati, ubao na vyombo vya kidijitali; kutoa mifano ya methali zinazohusu umoja na ushirikiano katika jamii; kusikiliza methali za umoja na ushirikiano zikitumiwa kupitia vyombo vya kidijitali; kujadili na wenzake maana na matumizi ya methali mbalimbali zinazohusu umoja na ushirikiano. | Je, ni nini umuhimu wa methali katika jamii?; Ni methali gani unazozijua kuhusu umoja na ushirikiano? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 1 | Kusikiliza Na Kuzungumza | Methali | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia methali zinazohusu umoja na ushirikiano katika mawasiliano; kuchangamkia matumizi ya methali zinazohimiza umoja na ushirikiano. | Mwanafunzi aelekezwe: kulinganisha methali na maana yake; kukamilisha methali mbalimbali zinazohusu umoja na ushirikiano katika mazungumzo akishirikiana na wenzake, kwenye daftari au kwa kutumia vyombo vya kidijitali; kusakura mtandaoni kwa kusaidiwa na mzazi au mlezi wake ili kupata methali zaidi zinazohusu umoja na ushirikiano na matumizi ya methali hizo, kujadili na wenzake kuhusu methali alizozipata mtandaoni ili wajengane kimaarifa. | Je, ni nini umuhimu wa methali katika jamii?; Ni methali gani unazozijua kuhusu umoja na ushirikiano? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 2 | Kusoma | Kusoma kwa Ufahamu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kujadili dhana za ukwapi na utao katika shairi ili kuzibainisha. | Mwanafunzi aelekezwe: kujadili ukwapi na utao katika shairi; kutambua ukwapi na utao katika shairi kwenye ubao, chati, vitabu au vyombo vya kidijitali; kusoma shairi akizingatia ukwapi na utao. | Je, kuna tofauti gani kati ya mashairi mbalimbali? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 3 | Kusoma | Kusoma kwa Ufahamu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua mashairi ya tathnia, tathlitha na tarbia kwa kuzingatia muundo; kusoma mashairi ya tathnia, tathlitha na tarbia ili kupata ujumbe. | Mwanafunzi aelekezwe: kujirekodi akisoma aina za mashairi lengwa akitumia vyombo vya kidijitali ili kuweza kujirekebisha anakokosea; kutofautisha mashairi ya tathnia, tathlitha na tarbia kwenye ubao, chati, vitabu au vifaa vya kidijitali; kutambua mashairi ya tathnia, tathlitha na tarbia katika matini mbalimbali; kusoma mashairi ya tathnia, tathlitha na tarbia kwa mahadhi mbalimbali. | Je, kuna tofauti gani kati ya mashairi mbalimbali? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 4 | Kusoma | Kusoma kwa Ufahamu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia usomaji wa mashairi ili kuyathamini. | Mwanafunzi aelekezwe: kujadili ujumbe kwenye shairi waliyoyasoma; kujibu maswali yanayotokana na mashairi aliyoyasoma; kuandika ujumbe alioupata katika mojawapo ya mashairi aliyoyasoma na kuujadili na wenzake darasani. | Je, kuna tofauti gani kati ya mashairi mbalimbali? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 1 | Kuandika | Insha za Maelezo | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua insha za maelezo katika matini mbalimbali; kuandika insha ya maelezo kwa kufuata kanuni zifaazo. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua vifungu vya maelezo vilivyoandikwa kwenye matini mbalimbali au tarakilishi; kujadili vidokezo vya insha ya maelezo atakavyovitumia katika kuandika insha yake. | Insha ya maelezo ina sifa gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 2 | Kuandika | Insha za Maelezo | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia utunzi bora maishani. | Mwanafunzi aelekezwe: kuonyesha umilisi wa ubunifu kwa kuandika insha ya maelezo (k.v. Siku ya sherehe ya kitaifa, Siku ya michezo ya kitaifa, Nchi yetu, n.k) isiyopungua maneno 200 akizingatia anwani, mpangilio mzuri wa mawazo, hati safi, tahajia, kanuni za kisarufi, uakifishaji mwafaka na lugha ya kiubunifu inayojumuisha methali na nahau alizojifunza awali ili kutoa picha dhahiri kuhusu anachokielezea; kukuza umilisi wa ujuzi wa kidijitali kwa kuandika insha ya maelezo na kuisambaza kwa wenzake na mwalimu ili kuisoma na kuitathmini. | Insha ya maelezo ina sifa gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 3 | SUamruilfiis i wa | Maw | Kujiamini | Ujuzi Maadili | Uwajibikaji | Uzalendo | Ngeli ya U- kUim singi unaokuzwan: asiliano na ushirikianaow – mwanafunzi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: w anafunzi anashirikiana anapotambua nomino za ngeli. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua viambishi vya ngeli ya U-U nak awtieknaz saeknet.e nsi kwa kuvipigia mstari yaa Uu -kUu vipikaosalevzyao r. angi katika tarakilishi, kuktaumtabmubau nao nmoimnoin zoa k nagtieklai ynag eUli- Uya. U-U kutokana naupatanisho wa kisarufi kwenye sentensi (k.m: uji, ugali, na wenzake. uhuru, ujanja, urafiki). | Je, ni nomino zipi hupatikana katika ngeli ya U-U? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 4 | SUamruilfiis i wa | Maw | Kujiamini | Ujuzi Maadili | Uwajibikaji | Uzalendo | Ngeli ya U- kUim singi unaokuzwan: asiliano na ushirikianaow – mwanafunzi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua viambishi n z i a n a p o t u m ia ta r akilishi. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua viambishi vya ngeli ya U-U nak awtieknaz saeknet.e nsi kwa kuvipigia mstari yaa Uu -kUu vipikaosalevzyao r. angi katika tarakilishi, kuktaumtabmubau nao nmoimnoin zoa k nagtieklai ynag eUli- Uya. U-U kutokana naupatanisho wa kisarufi kwenye sentensi (k.m: uji, ugali, na wenzake. uhuru, ujanja, urafiki). | Je, ni nomino zipi hupatikana katika ngeli ya U-U? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review |
Weeks 6–13 are in the full Term 2 document — KES 30 by M-Pesa.
Term 3 — Grade 6 Kiswahili scheme of work
13 weeks · first 5 freeStrands and sub-strands covered
| Wiki | Somo | Mada | Mada Ndogo | Matokeo Maalum Yanayotarajiwa | Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji | Swali Dadisi | Rasilimali za Ujifunzaji | Mbinu za Tathmini | Tafakari |
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | 1 | Sarufi | Ngeli ya PA-KU-MU (Kipindi 1) | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua nomino katika ngeli ya PA-KU-MU ili kuzibainisha; kuandika nomino za ngeli ya PA-KU-MU katika umoja na wingi. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua nomino katika ngeli ya PA-KU-MU kwenye kadi, mti wa maneno, tarakilishi au kapu la maneno (k.v: huku, humu, hapa, hapo, huko, humo, pale, kule, mle); kuandika nomino katika ngeli ya PA-KU-MU katika umoja na wingi akishirikiana na wenzake. | Nonimo katika ngeli ya PA-KU- MU ni gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 2 | Sarufi | Ngeli ya PA-KU-MU (Kipindi 1) | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuandika sentensi akitumia nomino za ngeli ya PA- KU-MU katika umoja na wingi akizingatia upatanisho wa kisarufi; kuchangamkia kutumia nomino za ngeli ya PA- KU-MU katika mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kubadilisha sentensi zenye nomino za ngeli ya PA-KU-MU katika umoja na wingi; kutunga sentensi kwa kutumia nomino ya ngeli ya PA-KU-MU akiwa peke yake au kwa kwa kushirikiana na wenzake; kujaza mapengo kwa kutumia viambishi vya ngeli ya PA-KU- MU kwa maandishi ya mkono au kwa tarakilishi. | Nonimo katika ngeli ya PA-KU- MU ni gani? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 3 | Kusikilizana Kuzungumza | Visawe | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua maneno zaidi ya matatu yenye maana sawa katika kundi la maneno; kutumia visawe ifaavyo katika mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua maneno zaidi ya matatu yenye maana sawa (k.v. mwizi-luja, mkupuzi, pwagu, pwaguzi, mkwepuzi; hongo, rushwa, chai, kadhongo, mvugulio; pesa - njenje, ngwenje, fedha, hela; lengo - dhamira, nia, azma, kusudi; maskini, mlalahoi, fukara, mkata, fakiri) kwa kutumia kapu la maneno, kadi za maneno, mti wa maneno, tarakilishi, n.k; kueleza maana ya maneno zaidi ya matatu yenye maana sawa kwa kujadiliana na wenzake; kuambatanisha maneno zaidi ya matatu yaliyo na maana sawa katika kapu la maneno, mti wa maneno, ubao, chati, vyombo vya kidijitali, kadi za maneno n.k. | Unajua maneno gani ya Kiswahili yaliyo na maana sawa? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 1 | 4 | Kusikilizana Kuzungumza | Visawe | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuthamini matumizi ya maneno zaidi ya matatu yenye maana sawa katika mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kuhusisha visawe na vifaa halisi, picha, michoro kwenye chati, kitabu au katika vyombo vya kidijitali; kujadili visawe mbalimbali akiwa na wenzake; kutumia kisawe kimoja kuchukua nafasi ya kingine katika sentensi. | Unajua maneno gani ya Kiswahili yaliyo na maana sawa? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 1 | Kusoma | Kusoma kwa Ufahamu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kujadili sifa za mchezo wa kuigiza ili kuzibainisha. | Mwanafunzi aelekezwe: kueleza maana ya mchezo wa kuigiza akishirikiana na wenzake; kujadili na wenzake sifa za mchezo wa kuigiza (k.v. huwa na wahusika, kuna mazungumzo, maelekezo); kusoma mchezo wa kuigiza akizingatia wahusika, maelekezo na ujumbe. | Je, mchezo wa kuigiza una sifa gani?; Umewahi kushiriki katika mchezo gani wa kuigiza? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 2 | Kusoma | Kusoma kwa Ufahamu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kusoma mchezo mfupi wa kuigiza kwa ufasaha kwa kuzingatia ujumbe na msamiati wa suala lengwa; kuonyesha ufahamu wa mchezo wa kuigiza kwa kujibu maswali na kutoa muhtasari. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua msamiati wa suala lengwa uliotumiwa katika mchezo wa kuigiza (k.v. kiboko, samaki, mamba, chura, kasa); kushiriki katika majadiliano kuhusu msamiati uliotumiwa katika mchezo wa kuigiza, kujibu maswali kutokana na mchezo aliousoma. | Je, mchezo wa kuigiza una sifa gani?; Umewahi kushiriki katika mchezo gani wa kuigiza? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 3 | Kusoma | Kusoma kwa Ufahamu | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuonea fahari nafasi ya mchezo wa kuigiza katika jamii. | Mwanafunzi aelekezwe: kutoa muhtasari wa ujumbe ulio katika mchezo wa kuigiza; kutazama mchezo mfupi wa kuigiza shuleni au kwenye vifaa vya kidijitali; kushiriki katika mjadala kuhusu ujumbe unaojitokeza kwenye mchezo wa kuigiza. | Je, mchezo wa kuigiza una sifa gani?; Umewahi kushiriki katika mchezo gani wa kuigiza? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 2 | 4 | Kuandika | Insha za Masimulizi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kujadili mtiririko wa hoja katika insha ya masimulizi; kuandika insha ya masimulizi kwa kufuata kanuni zifaazo. | Mwanafunzi aelekezwe: kujadili mtiririko wa hoja katika insha ya masimulizi kwa kurejelea vielelezo vya insha zilizoandikwa kwenye matini mbalimbali au tarakilishi; kujadili muundo wa insha ya masimulizi. | Ni nini unachoweza kufanya ili uwe mwandishi bora wa insha? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 1 | Kuandika | Insha za Masimulizi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia utunzi mzuri katika uandishi wa insha ya masimulizi. | Mwanafunzi aelekezwe: kuonyesha ubunifu kwa kuandika insha isiyopungua maneno 200 inayosimulia tukio linalohusiana na wanyama wa porini akizingatia nomino na vivumishi mbalimbali, mnyambuliko wa vitenzi, anwani, mpangilio mzuri wa mawazo, hati safi, tahajia, kanuni za kisarufi, uakifishaji mwafaka, lugha ya kiubunifu na urefu unaotarajiwa; kukuza ujuzi wa kidijitali kwa kuandika insha ya masimuizi katika vifaa vya kidijitali na kuisambaza kwa wenzake na mwalimu ili kuisoma na kuitathmini; kuwawasilishia wenzake insha aliyoandika ili waitathmini na kumwelekeza. | Ni nini unachoweza kufanya ili uwe mwandishi bora wa insha? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 2 | Sarufi | Mnyambuliko wa Vitenzi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua vitenzi katika hali ya kutendeana, kutendesha, kutendua katika matini. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua vitenzi katika hali za kutendeana, kutendesha na kutendua katika chati, jedwali, kapu la maneno, mti wa maneno, ubao na vyombo vya kidijitali; kunyambua vitenzi katika hali lengwa akiwa peke yake, akishirikiana na wenzake. | Je, vitenzi vinaweza kubadilika vipi mwishoni ili kuleta maana mbalimbali? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 3 | Sarufi | Mnyambuliko wa Vitenzi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutumia vitenzi katika hali za kutendeana, kutendesha, kutendua ipasavyo katika sentensi. | Mwanafunzi aelekezwe: kutumia vitenzi katika hali lengwa kwenye sentensi. | Je, vitenzi vinaweza kubadilika vipi mwishoni ili kuleta maana mbalimbali? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 3 | 4 | Sarufi | Mnyambuliko wa Vitenzi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia matumizi ya vitenzi katika hali ya kutendeana, kutendesha, kutendua katika mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kujaza mapengo katika jedwali la mnyambuliko we vitenzi kwenye daftari au kwa kutumia tarakilishi; kuandika sentensi upya kwa kutumia vitenzi katika hali mbalimbali. | Je, vitenzi vinaweza kubadilika vipi mwishoni ili kuleta maana mbalimbali? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 1 | Kusikilizana Kuzungumza | Mazungumzo ya Kimuktadha | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua miktadha rasmi na isiyo rasmi katika mawasiliano ili kuitofautisha; kutumia lugha katika miktadha rasmi na isiyo rasmi ili kufanikisha mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua miktadha mbalimbali kunakotumiwa lugha rasmi na isiyo rasmi (k.v. ofisini, hospitalini, nyumbani, sokoni); kusikiliza mazungumzo rasmi na yasiyo rasmi kwa kutazama maigizo kwenye vyombo vya kidijitali (k.v. video, rununu, runinga, tarakilishi. | Ni wapi katika shughuli zetu za kila siku tunaitumia lugha rasmi na isiyo rasmi?; Ni nini kinachofanya mazungumzo yawe rasmi au yasiyo rasmi | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 2 | Kusikilizana Kuzungumza | Mazungumzo ya Kimuktadha | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: Kuchangamkia matumizi ya lugha katika miktadha rasmi na isiyo rasmi kuimarisha maadili yafaayo. | Mwanafunzi aelekezwe: kushiriki katika maigizo ya mazungumzo ya miktadha rasmi na yasiyo rasmi akishirikiana na wenzake; kushiriki katika mazungumzo rasmi nje ya darasa k.m. akiwa kwenye gwaride, majilisini n.k na yale yasiyo rasmi kama vile uwanjani, kwenye bweni, katika safari ya kwenda nyumbani kutoka shuleni; kutambua nidhamu ya lugha inayozingatiwa katika mazingira rasmi (k.m lugha ya heshima na adabu anapowasiliana). | Ni wapi katika shughuli zetu za kila siku tunaitumia lugha rasmi na isiyo rasmi?; Ni nini kinachofanya mazungumzo yawe rasmi au yasiyo rasmi | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 3 | Kusoma | Kusoma kwa Mapana | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua aina mbalimbali za matini ili kuchagua inayomvutia. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua matini zinazomvutia maktabani na mtandaoni. | Ni habari zipi unazopenda kusoma kwenye matini?; Unazingatia nini unapochagua matini za kusoma? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 4 | 4 | Kusoma | Kusoma kwa Mapana | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kusoma matini aliyochagua ili kufaidika na ujumbe na lugha iliyotumiwa. | Mwanafunzi aelekezwe: kusoma matini alizochagua ili kufaidi ujumbe na lugha iliyotumiwa; kutoa wenzake muhtasari wa kile alichosoma kwenye matini ili kupashana ujumbe na kuchocheana kusoma zaidi kwa ajili ya kujifurahisha. | Ni habari zipi unazopenda kusoma kwenye matini?; Unazingatia nini unapochagua matini za kusoma? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 1 | Kusoma | Kusoma kwa Mapana | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kufurahia usomaji wa aina mbalimbali za matini ili kupanua mawazo yake. | Mwanafunzi aelekezwe: kujadiliana na wenzake matini ambazo wamesoma kwa kuzingatia ukuzaji wa msamiati. | Ni habari zipi unazopenda kusoma kwenye matini?; Unazingatia nini unapochagua matini za kusoma? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 2 | Kuandika | Insha za Maelezo | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kueleza maudhui ya insha ya maelezo kwa kuzingatia mada; kuandika insha ya maelezo kwa kufuata kanuni zifaazo ili kufanikisha, mawasiliano. | Mwanafunzi aelekezwe: kukuza uwazaji kina na utatuzi wa matatizo kwa kueleza; maudhui kutokana na mada ya insha ya maelezo; kujadili mada ya insha na muundo wa insha ya maelezo. | Je, ni mada gani | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 3 | Kuandika | Insha za Maelezo | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kuchangamkia utunzi mzuri wenye mapambo ya lugha. | Mwanafunzi aelekezwe: kuandika insha ya maelezo akitumia vivumishi na vielezi vifaavyo kutoa picha dhahiri kuhusu anachokielezea. Pia akizingatie anwani, mpangilio mzuri wa mawazo, hati safi, kanuni za kisarufi, uakifishaji mwafaka na lugha ya kiubunifu inaojumuisha methali na nahau alizojifunza awali; kukuza umilisi wa ujuzi wa kidijitali kwa kuandika insha ya maelezo mtandaoni na kuisambaza kwa wenzake na mwalimu ili kuisoma na kuitathmini; kuwawasilishia wenzake insha aliyoandika ili waitathmini. | Je, ni mada gani | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review | |
| 5 | 4 | Sarufi | Vinyume vya Vivumishi | Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze: kutambua vinyume vya vivumishi katika matini; kutunga sentensi kwa kutumia vinyume vya vivumishi. | Mwanafunzi aelekezwe: kutambua vinyume vya vivumishi (k.v. zuri-baya, kali-butu, refu-fupi) katika chati, kadi za maneno, kapu la maneno, mti wa maneno au vifaa vya kidijitali; kutafuta vinyume vya vivumishi kwa kurejelea orodha ya vivumishi alivyopewa. | Je, ni vivumishi vipi unavyoweza kutambua vinyume vyake? | Kitabu cha mwanafunzi, chati, kadi za maneno, rekodi za sauti, kifaa cha kidijitali | Observation, oral questions, written exercises, group discussion, project work and portfolio review |
Weeks 6–13 are in the full Term 3 document — KES 30 by M-Pesa.
More Grade 6 schemes of work
Questions about this scheme of work
Does this page cover all the terms?
It carries Terms 1, 2 and 3 of 2026 — every term published for Grade 6 Kiswahili so far. Each term has its own week-by-week table and free preview, and a new term joins this same page when it goes live.
How do I download a whole term as a PDF?
The first 5 weeks of each term are free to read on this page. Open the term you need, pay KES 30 by M-Pesa, then use Print / Save PDF — the sheet is laid out for A4 landscape.
Can I adapt it for my own school calendar?
Every scheme is generated from the curriculum taxonomy, so you can rebuild it with your own week count, strands and pacing on the Generate screen and keep the result as your own document.